Mhe. Balozi Elsie Kanza amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Joy Basu, Naibu Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje (DAS) wa Marekani, anayeshughulikia masuala ya Uchumi, Ofisi ya Afrika. Mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye biashara na uwekezaji wa sekta binafsi katika miundombinu, kilimo na nishati. Walijadili pia fursa zinazopatikana katika taasisi za Serikali ya Marekani za EXIM bank, DFC na USTDA.