Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza amekutana na kufanya mazungumzo na wanachama wa Young Presidents’ Organisation (YPO) kwenye hafla ya Chakula cha Jioni iliyofanyika hapa Ubalozini.  Mhe. Balozi alitumia hafla hiyo kuwaelezea wanachama hao wa YPO kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania katika sekta za kipaumbele ikiwemo kilimo, uchukuzi, nishati, madini, TEHAMA, afya na utalii. Vilevile, aliwakaribisha wanachama hao wa YPO kutembelea Tanzania na kuchangamkia fursa hizo ambapo walionesha utayari wa kufanya hivyo.  YPO ni taasisi inayojumuisha wafanyabiashara na viongozi waandamizi wa kampuni mbalimbali wenye mafanikio ya kiutendaji kutoka sekta tofauti. Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1950 hapa Marekani na sasa ina zaidi ya wanachama 35,000 kutoka zaidi ya nchi 140 duniani.