Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, amezungumza na baadhi ya wadau wa sekta ya uwindaji kutoka Tanzania na Marekani, wakati wa maonesho ya uwindaji jijini Dallas, Texas. Lengo la mazungumzo hayo ni kuiboresha zaidi sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi yetu na uhifadhi wa wanyama na mazingira yake. Wawindaji wengi wanaokuja Tanzania hutokea Marekani.