Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza akizungumza na Bw. Matt Damon, Muigizaji Maarufu duniani ambaye pia ni mwanzilishi mwenza wa taasisi za Water.org na WaterEquity pamoja na Bw. Gary White, mwanzilishi mwenza wa taasisi hizo. Mhe. Balozi alikuwa amealikwa kushiriki kwenye hafla ya utoaji tuzo ya mwaka 2024 ya J. William Fulbright Prize for International Understanding ambayo ilitolewa kwa Bw. Damon na Bw. White kutokana na mchango wa taasisi tajwa walizoziasisi katika kuleta maji safi kwenye nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.