Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alifanya mazungumzo na uongozi wa Shule ya Utabibu ya Chuo Kikuu cha Emory jijini Atlanta, Georgia alipokuwa jijini humo kushiriki kwenye Tamasha la Wanadiaspora wa Tanzania wa DICOTA (Urithi Fest 2025). Mhe. Balozi na uongozi wa chuo hicho walijadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano, ikiwemo fursa za masomo na mafunzo kwa Watanzania na ushirikiano wa kitaasisi baina ya Chuo hicho na vyuo vya Tanzania. Mwanadiaspora, Dkt. Frank Minja, ambaye pia ni Rais wa Jumuiya ya Watanzania Georgia ni profesa kwenye Chuo hicho.