Tarehe 15 Mei 2024 Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikutana na kufanya mazungumzo na Bi. British A. Robinson, Mratibu wa Taasisi ya Serikali ya Marekani ya Prosper Africa. Madhumuni ya mazungumzo hayo ni kujadiliana namna Ubalozi unavyoweza kishirikiana na taasisi hiyo kuhamasisha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani. Mhe. Balozi alikueleA Bi. British vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Sita hususan kwenye biashara na uwekezaji. Bi. Robinson kwa upande wake, alieleza utayari wa Prosper Africa kushirikiana na Ubalozi. Alieleza zaidi kuwa mwaka huu timu ya watu wachache kutoka Prosper Afrika watafanya ziara nyumbani kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu biashara na uwekezaji.