Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mgeni mzungumzaji kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyoandaliwa na taasisi ya Business Council for International Understanding (BCIU) ya hapa Marekani kwa kushirikiana na Jumuiya ya Mabalozi wa Afrika wanaoziwakikisha nchi zao Marekani (ADC). Kwenye hotuba yake, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi alizungumzia jitihada za Serikali katika kupambana na VVU/UKIMWI, alishukuru mchango wa Washirika wa Maendeleo ikiwepo Serikali ya Marekani hasa kupitia mpango wake wa PEPFAR katika mapambano hayo na alieleza kuhusu mpango wa Serikali kujitegemea zaidi katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mabalozi; Viongozi wa Serikali ya Marekani akiwemo Dkt. John Nkengasong, Mratibu wa Masuala ya Ukimwi wa Serikali ya Marekani; Wabunge wa Bunge la Marekani; Sekta Binafsi; Taasisi zisizo za Kiserikali; Vyuo Vikuu na Mashirika ya Kimataifa.