Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu kwenye mkutano uitwao Executive Networking Conference ulioandaliwa na taasisi ya Minority Instutitute of Economic Development (NIMED) katika mji wa Pinehurst, North Carolina kuanzia tehere 11 hadi 13 Agosti 2025 kwa lengo la kufungua fursa za kibiashara kwa wanachama wa taasisi hiyo. Akizungumza kwenye mkutano huo, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi aliwaeleza washiriki kuhusu mafanikio yaliyopatikana katika kongamano lililofanyika mwezi Machi 2025 jijini Dar es salaam Dar es salaam chini ya uratibu wa Ubalozi kwa kushirikiana na taasisi hiyo, ambapo alibainisha kuwa kampuni tatu (3) kati ya 12 zilizoshiriki kongamano hilo kutoka Marekani zipo katika mbalimbali za kukamilisha makubaliano ya kibiashara nchini Tanzania.
Mheshimiwa Balozi pia alielezea
fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana kwenye sekta za vipambele nchini Tanzania ikiwemo chakula na kilimo biashara, utalii, madini, madini, usafirishaji na nishati safi. Vile vile, alibainisha sababu zinazoifanya Tanzania kuwa sehemu bora zaidi kufanya biashara na uwekezaji barani Afrika na aliwakaribisha kufanya ziara nchini Tanzania ili kuchangamkia fursa zilizopo na kutembelea vivutio vya utalii.
Aidha, kwenye mkutano huo baadhi ya walishiriki wa kongamano lililofanyika mwezi Machi jijini Dar es salaam walitoa uhushuda wa fursa zilizopo nchini Tanzania pamoja na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji na kuwashauri washiriki wengine kuitembelea Tanzania ili kujionea wenyewe.


