Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa ni miongoni mwa wazungumzaji katika Jukwaa liitwalo Global Black Economic Forum (GBEF) ambalo ni sehemu ya tamasha maarufu la Essence (Essence Festival of Culture) lililofanyika New Orleans, Louisiana mwezi Julai 2025. Akizungumza kwenye Jukwaa hilo, pamoja na masuala mengine, Mhe. Balozi aliwaeleza washiriki kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini Tanzania, sababu zinazoifanya Tanzania kuwa sehemu bora zaidi kufanya biashara na uwekezaji barani Afrika na aliwakaribisha kufanya hivyo. Mhe. Balozi aliwakaribisha pia kutembelea Tanzania na kujionea vivutio vizuri na vya kipekee vilivyopo.

Pembezoni mwa Jukwaa hilo, Mhe. Balozi alifanya mazungumzo na viongozi mbalimbali na kujadiliana nao maeneo tofauti ya ushirikiano. Viongozi hao ni pamoja na Mhe. JB Pritzker, Gavana wa jimbo la Illinois; Bw. Alphonso Davis, Mkurugenzi Mtendaji wa GBEF; na Balozi Ron Kirk, aliyekuwa Mwakilishi wa Marekani wa Masuala ya Biashara na Meya wa zamani wa jiji la Dallas.