Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na Bw. Vincent D. Spera, Naibu Waziri Mdogo (Deputy Assistant Secretary) kwenye Ofisi ya Masuala ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kujadili masuala mbalimbali muhimu yanayolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani.

