Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na Mhe. Jonathan Jackson, Mbunge wa Bunge la Wawakilishi la Marekani kutoka Jimbo la Illinois ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Afrika ya Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge hilo. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa ni kufahamiana na kujadili masuala tofauti yanayohusu uhusiano baina ya Tanzania na Marekani ikiwemo sera mbalimbali zinazohusu uhusiano huo pamoja athari zinazoweza kutokana na sera hizo. Aidha, Viongozi hao walikubaliana kuendelea kushirikiana kwa lengo la kuimarisha zaidi uhusiano baina ya Tanzania na Marekani.