Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Wilbard Shihepo Manique Hellao, Balozi Mpya wa Namibia nchini Marekani. Pamoja na masuala mengine, lengo la kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kujadili masuala yanayohusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo rafiki. Kadhalika, kikao kilijadili ajenda mbalimbali zinazolenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi za Afrika na Marekani.