Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki kwenye hafla ya kusheherekea msimu wa Sikukuu iliyoandaliwa na Mhe. Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwa ajili ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Marekani. Hafla hiyo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo na taifa la Marekani.