Mhe.  Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza ameshiriki katika ufunguzi wa Ofisi ya Biashara ya Tanzania jijini Dallas chini ya Mpango wa  “Foreign Trade Offices Initiative” wa jiji hilo.  Ofisi hiyo itakayoendeshwa na “Tanzanian American Chamber of Commerce” itaongeza nguvu jitihada za Ubalozi za kuongeza biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Marekani kwa kuzingatia nafasi ya jiji la Dallas kama kitovu cha biashara na usafirishaji, na ni  miongoni mwa majiji yenye uchumi mkubwa na uonakua kwa kasi duniani.

Uzinduzi huo umehudhuriwa viongozi mbalimbali wakiwemo Meya wa jiji la Dallas, Mhe. Eric L. Johnson; Mkurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Bi. Katherine Ho; na Bi. Florie Liser, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Corporate Council on Africa.