Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alifanya ziara ya kikazi jijini Washington, D.C., Marekani na kukutana na wadau mbalimbali muhimu katika kuimarisha uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na Marekani.

Akiwa nchini Marekani, pamoja na masuala mengine, Mhe. Waziri alikutana kwa mazungumzo na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Marekani. Miongoni mwa viongozi aliokutana nao ni Mhe. Brian J. Mast, Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani.