Mhe. Dkt. Elsie Sia Kanza amekutana kwa mazungumzo na viongozi waandamizi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Compassion International. Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Ubalozi hapa Washington, D.C. yalijadili, pamoja na masuala mengine, shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo nchini Tanzania ikiwemo mipango ya kuzipanua zaidi.

Taasisi ya Compassion International ni taasisi ya hisani ya Kikristo iliyojikita kwenye shughuli mbalimbali zinazohusu watoto kwa lengo la kuondoa umaskini kwa watoto kwa kutoa huduma za maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidini. Taasisi hiyo yenye makao makuu jimbo la Colorado hapa Marekani imeanza shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1999.