Kabla ya kuanza kwa mikutano ya Majira ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF, Mhe. Balozi Dkt. Elsie S. Kanza alifanya mkutano kwa njia ya mtandao na wanadiaspora wa Tanzania wanaoishi nchini Marekani na Mexico, tarehe 19 Aprili 2025. Kwenye Mkutano huo uliokuwa wa pili ndani ya mwaka huu, Ubalozi ulitoa taarifa mbalimbali muhimu kwa diaspora zinazohusu maslahi na ustawi wao, na kwa upande wao, diaspora walitoa mchango wao kuhusu masuala tofauti yanayolenga kuchangia maendeleo ya Taifa. Kwa ujumla wake, mkutano uliazimia Ubalozi kama mlezi wa diaspora  kuendelea kushirikiana na wanadiaspora kwa manufaa ya Taifa, wanadiaspora na Watanzania wote.