Ubalozi ulishirikiana na Programu ya Afrika ya taasisi ya Carnegie Endowment for International Peace (CEIP) kuandaa mkutano uliojadili uhusiano wa kibiashara baina ya Marekani na Afrika, mnyororo wa ugavi wa madini adimu na uhusiano baina ya nchi za Afrika na Serikali ya Marekani.
Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza alikuwa mwenyekiti mwenza wa Mkutano huo ambapo aliongoza pia mjadala husika. Mwenyekiti mwenza mwingine alikuwa ni Dkt. Zainab Usman, Mkurugenzi wa Programu ya Afrika ya CEIP. Mkutano huo ulihusisha Mabalozi wa nchi za Kiafrika na wawakilishi wao.
Pamoja na masuala mengine, kwenye Mkutano huo, Mabalozi walisisitiza nia yao thabiti ya kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri na Serikali ya Marekani na kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayogusa maslahi ya pande zote mbili ikiwemo biashara, uwekezaji, uchumi na diplomasia.