Ubalozi ulishiriki kuwaunga mkono wanafunzi wa Kitanzania kutoka Dar es Salaam Independent School ambao walikuja jijini New Haven, CT, hapa Marekani kushiriki kwenye mashindano ya World Scholar’s Cup yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Yale. Tulifurahi kushuhudia wanafunzi hao wakishinda tuzo 8 za dhahabu na 33 za fedha. Tunawapongeza sana.


