Ubalozi ulishiriki kwenye programu iitwayo Around the World Embassy Tour - Passport DC 2026 na kukaribisha takribani wageni 2,000 waliokuwa na shauku ya kujifunza kuhusu utamaduni, vivutio vya utalii na fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania. Kadhalika, wanadiaspora wa Tanzania walionesha na kuuza bidhaa mbalimbali za Kitanzania kwa wageni. Wageni hao walifurahi kutembelea Ubalozi na kuahidi kutembea Tanzania ili kujionea moja kwa moja tamaduni na vivutio vilivyopo.



