Ubalozi uliungana na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi jiji la Chicago na maeneo ya jirani kwenye sherehe za kuadhimisha Uhuru wa Tanzania Bara. Bi. Sophia Gunda, Afisa Mwandamizi wa Ubalozi aliuwakilisha Ubalozi kwenye sherehe hizo na kutoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Balozi. Pamoja na diaspora wa Tanzania, sherehe hizo zilihudhuriwa pia na marafiki mbalimbali wa Tanzania na mwakilishi kutoka ofisi ya Meya wa Chicago. Wakati wa maadhimisho hayo, kulikuwa pia na maonesho ya utamaduni wa Tanzania na vivutio vya utalii vya Tanzania. Tunawatakia wote Heri ya Siku ya Uhuru.